
Hizi Beef ambazo zimetajwa kuwa za kitoto kwenye hiphop.
Beef ya rapper Tyga na Drake iliyotokana na Tyga kusema hampendi Drake kwamba sio mtu REAL.
Floyd Mayweather alisema 50 Cent hana
seheu tena kwenye muziki wa rap na hana album inayofanya vizuri
sokoni.Baadae 50 Cent alianzisha kampuni ya kusimamia mapambano ya
ngumi.
Ndio beef ya rap yenye umaarufu zaidi kwa
sasa, Drake na Chris brown hawaelewani baada ya kumpigania Rihanna
mwaka 2012 na sasa Drake amelaumiwa tena na Chris Brown kwa kumchukua
mpenzi wake K Tran.
Meek Mil alilalamika kuwa pamoja na kuwa
kwenye lebel moja na Wale, jamaa hajamsaidia kutangaza album yake kwenye
twitter wale kwenye interview zake, Meek anaamini Wale anamchukia.
Drake na Common wote wanampenda mwanamke moja ‘ Serena Williams’ mcheza tennis maarufu duniani.
Manager wa Justin Bieber ‘Scooter’
alimwambia msanii wake asifuatane na rapper wa Young Money ‘Lil Twist’
sababu hana nidhamu na atamfundisha tabia mbaya.
Wakati Jay Z yuko mapumziko mshkaji wa
rappa Cam’ron ‘Jim Jones’ alitangaza kuwa makamu wa rais waRoc-A-Fella
records atakuwa Cam’ron na ameteuliwa na Dame Dash ambaye kwa wakati
huo alikuwa mmiliki wa lebel hio akishirikiana na Jay Z. Miezi michache
baadae Dash aliuza hisa zake na Jay Z akawa mmiliki bila kumpa cheo
chochote Cam’ron.
Meek Mill na Cassidy walipishana baada ya
Meek kusema anaweza kushinda Freestyle na Cassidy. Haikwenda mbali
baada ya Meek kuambiwa kuwa hawezi kushinda na atapoteza heshima kama
atashindwa na Cassidy.
No comments:
Post a Comment